Viongozi wa dunia wampongeza Biden, wataka umoja
8 Novemba 2020Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alikuwa miongoni mwa viongozi wa kwanza kabisaa kumpongeza Biden na Kamala Harris, katika taarifa, akisema anatazamia kushirikiana pamoja na viongozi hao wateule.
Peter Beyer, mratibu wa serikali ya Ujerumani wa ushirikiano wa kanda ya Atlantiki, alisema inagawa kura zote zilikuwabado hazijahesabiwa, "tunaweza kumpongeza rais mteule Joe Biden na kwamba ishara kubwa ya pumzi inaonekana kote duniani."
Soma pia: Maoni: Rais mpya - lakini hakuna mshindi
Salaam za pongezi zimetoaka miji mikuu ya dunia, viongozi wakipuuza madai ya Trump kwamba uchaguzi huo ulioonesha migawiko mikubwa ulikuwa hujaisha. Beyer alisema kwamba Ujerumani imekuwa na wakati mgumu hasa wakati wa miaka minne ya itawala wa Trump, na kuongeza kwamba anatazamia kushirikiana na utawala mpya.
"Kuna ahueni baada ya uzoefu tuliokuwa nao katika miaka minne iliyopita, kwamba mawasiliano ya mataifa ya kanda ya Atlantiki na ushirikiano viliharibika vibaya," alisema mbunge huyo wachama cha kansela Angel Merkel cha CDU.
"Tulikuwa na wakati mkgumu sana na jukumu na changamoto vilivyopo mbele yetu ni vikubwa sana hivyo natazamia kuboresha ushirkkiano na utawala mpya."
Matumaini ya mwanzo mpya
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema katika ujumbe wa Twitter kwamba Wamarekani wamemchagua rais wao. "Hongera Biden na Kamala Harris. Tuna mengi ya kufanya kushughulikia changamoto za sasa. Tushirikiane pamoja.!"
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson pia alimpongeza Biden na Kamala, na kusema Marekani ndiyo mshirika muhimu zaidi wa Uingereza na anatazamia kufanya kazi kwa karibu zaidi juu ya vipaumbele vyao vya pamoja, kuanzia mabadiliko ya tabianchi, hadi biashara na usalama.
Soma pia:Biden, Harris watoa hotuba ya shukrani kwa ushindi wa kishindo, bado Trump hajayatambua matokeo
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, mshirika wa karibu wa rais Trump, amemtaja Biden kuwa rafiki mkubwa wa Israel, na kumpongeza yeye pamoja na Harris juu ya ushindi wao. Alisema katikaujumbe wa twitter: "Natazamia kufanya kazi pamoja na nyote wawili kuimarisha zaidi ushirikiano maalumu kati ya Marekani na Israel."
Mfalme wa Jordan, Abdullah II, pia alitumia mtandao wa Twitter kuwapongeza washindi hao wawili akisema, "natazamia kushirkiana nanyi kuendeleza ushirkiano imara kati ya Jordan na Marekani, katika kuendeleza malengo yetu ya pamoja ya amani, utulivu na ustawi."
Waziri mkuu wa Canada Justion Treduea, alisema pia anatazamia kushirikiana na rais mteule Biden na makamu wake Harris, utawala wao na bunge la Marekani wakati wakishughulikia changamoto kubwa zaidi za dunia.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, alitoa wito wa ushirikishwaji zaidi wa bara la Afrika. Alisema anatazamia ushirikiano zaidi kati ya Nigeria na Marekani, hasa katika ngazi za uchumi, diplomasia na siasa, ikiwemo kuhusu vita dhidi ya ugaidi.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, alisema kupitia Twitter kwamba serikali yake inatazamia kufanyakazi pamoja na viongozi ho wateule, kuimairsha urafiki na ushirikiano.
Soma pia Joe Biden ni rais mteule wa Marekani
Rais wa Mexico Manuel Lopez Obrador hata hivyo alisema ni mapema mno kumpongeza Biden na kwamba atasubiri hadi masuala yote ya kisheria kuhusu uchaguzi huo yatatuliwe.
Kwa upande wake, katibu mkuu wa jumuiya ya kujihami NATO, Jens Stoltenberg, amemuelezea Biden kama muungaji mkono thabiti wa muungano huo.
Stoleteberg, ambaye mara nyingi alilaazimika kuzowea tabia ya Trump ya kutoa matangazo ya ghafla kuhusu kupunguza vikosi vya Marekani vinavyohudumu katika jumuiya ya NATO, alisema anatazamia kushirikiana na Biden.
Chanzo: Mashirika