1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa dunia kuhutubia Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa

24 Septemba 2024

Viongozi wa serikali na mataifa wanachama wa Umoja wa Mataifa wanaanza wiki moja ya mkutano wa hadhara kuu ya Umoja huo hivi leo, ambapo vita vya Gaza, Lebanon, Sudan na Ukraine vinatarajiwa kuchukuwa sehemu kubwa.

https://p.dw.com/p/4kzyc
Mkutano wa Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa.
Mkutano wa Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa.Picha: Selcuk Acar/Andalou/picture alliance

Zaidi ya wakuu 100 wa mataifa na serikali wamepangiwa kuhutubia kwenye jukwaa hilo muhimu la ulimwengu kuanzia leo hadi Jumatatu ijayo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameonya kwamba changamoto za kimataifa zinasonga mbele kwa kasi zaidi kuliko uwezo wa chombo chake kuzitatuwa.

Soma zaidi: Viongozi wa dunia kuhutubia Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa

Kutokana na Umoja huo kushindwa kukomesha mauaji kwenye mizozo inayoendelea sasa ulimwenguni, baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kimataifa wanasema Umoja wa Mataifa unaelekea kutokuwa na nafasi yoyote kwenye siasa wala usalama wa dunia.