1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMarekani

Vimbunga vyasababisha vifo vya watu 26 Mississippi, Marekani

26 Machi 2023

Watu wasiopungua 26 wamekufa kufuatia vimbunga vilivyoshuhudiwa katika Jimbo la kusini mwa Marekani la Mississippi. Nyumba, magari na miundombinu kadhaa vimeharibiwa vibaya.

https://p.dw.com/p/4PFya
USA | Schäden nach Tornado in Mississippi
Picha: Lokman Vural Elibol/AA/picture alliance

Hali mbaya zaidi ya hewa ikiambatana na mvua kubwa na upepo mkali inatarajiwa hii leo huko Mississippi. Shirika la usimamizi wa dharura la serikali limeonya kwamba huenda kukashuhudiwa pia vimbunga.

Baadhi ya vitongoji vimeathirika pakubwa ikiwemo kile cha Rolling Fork chenye wakazi wasiozidi 2000, ambako majengo yote yameteketea. Watu wapatao 4,800 hawakuwa na umeme huko Mississippi huku kaya 11,000 zikikosa umeme katika eneo jirani la Alabama.

Soma pia: Kimbunga chauwa zaidi ya watu 70 Marekani

Rais Joe Biden amesema hali huko Mississippi ni ya kuvunja moyo na kuapa kufanya kila liwezekanalo ili kutoa msaada kwa waathiriwa wa vimbunga hivyo. Vimbunga huripotiwa mara kwa mara nchini Marekani hasa katika maeneo ya kati na kusini mwa nchi hiyo.