1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya Ukraine vyakabiliana na vikosi vya Urusi Donetsk

27 Agosti 2022

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema katika siku tano zilizopita, kuna uwezekano Urusi imezidisha mashambulizi yake katika eneo la Donetsk mashariki mwa Ukraine kwenye mkoa wa Donbas.

https://p.dw.com/p/4G8Fy
Ukraine | Russische Soldaten am Atomkraftwerk in Saporischschja
Picha: AP/picture alliance

Siku ya Jumamosi mamlaka ya kijeshi ya Ukraine imeeleza kuwa vikosi vyake viliwarejesha nyuma wanajeshi wa Urusi katika maeneo ya Soledar, Zaitseve na Mayorsk katika mkoa wa Donetsk.

Katika hotuba yake kwa njia ya video jana usiku, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema hali bado ni tete na ya hatari mno katika kituo cha nyuklia kinachodhibitiwa na Urusi cha Zaporizhzhia.

Naye, Rais wa zamani wa Urusi Dmitry Medvedev, ambaye ni mshirika mkuu wa Rais Vladimir Putin, amesema Moscow haitasitisha harakati zake za kijeshi nchini Ukraine licha ya Kyiv kutangaza rasmi kuachana na dhamira yake ya kujiunga na Jumuiya ya Kujihami ya NATO.