1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya Marekani vyaondoka nchini Niger

8 Julai 2024

Wanajeshi wa Marekani wamekamilisha mchakato wa kuondoka katika kambi yao kwenye mji mkuu wa Niger, Niamey na wataondoka kikamilifu kutoka eneo la Agadez kaskazini mwa nchi hiyo kabla ya tarehe ya mwisho ya Septemba 15

https://p.dw.com/p/4i0qZ
Niger, Niamey | kuondoka kwa jeshi la Marekani Niamey
Kiongozi wa jeshi la Marekani nchini Niger, Jenerali Kenneth Ekman Picha: ISSIFOU DJIBO/EPA

Katika taarifa, nchi hizo mbili zimesema kuwa wizara ya ulinzi ya Niger na Idara ya Ulinzi ya Marekani zimetangaza kukamilika kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani na vifaa kutoka kambi 101 huko Niamey.

Ndege ya mwisho iliyobeba wanajeshi wa Marekani ilitarajiwa kuondoka Niamey jana jioni.

Ujumbe wa Marekani wajadili kuondoka kwa wanajeshi Niger

Siku ya Jumamosi, wizara ya ulinzi ya Ujerumani pia ilisema itakamilisha operesheni zake katika kambi yake nchini Niger kufikia Agosti 31 kufuatia kuvunjika kwa mazungumzo na viongozi wa kijeshi.