Syria yajipanga kulipiza mashambilio ya waasi mkoani Hama
3 Desemba 2024Matangazo
Wakati huohuo Qatar kupitia msemaji wa wizara yake ya mambo ya kigeni imesema inashirikiana na Uturuki pamoja na washirika wengine wa kikanda kutafuta suluhisho la kumaliza mapigano Syria.
Vikosi vya Syria vyashambulia vijiji kaskazini mwa Syria na kuongeza wasiwasi kwa jirani yake, Iraq
Kuafuatia mapigano yaliyoibuka nchini Syria, Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk ameelezea wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa vita Kaskazini magharibi mwa Syria.
Ameyasema hayo huku ofisi yake ikitafuta taarifa kuthibitisha idadi ya mashambulio ya umwagaji damu yaliyofanywa na pande zote mbili, vikosi vya jeshi la serikali na waasi.