1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Vijana 12 wa Israel wauawa kwa shambulizi la roketi

28 Julai 2024

Waziri wa ulinzi wa Israel Yoav Gallant ameapa kumshambulia vikali ''adui'' baada ya shambulizi la kombora kutoka Lebanon kuwaua vijana 12 katika eneo la milima ya Golan.

https://p.dw.com/p/4ipmV
Shambulizi la roketi katika uwanja wa mpira mjini Druze, Majdal Shams mnamo Julai 27,2024
Shambulizi la roketi katika uwanja wa mpira mjini Druze, Majdal ShamsPicha: Hassan Shams/AP/picture alliance

Jeshi la ulinzi la Israel limesema shambulizi hilo la kombora katika mji wa Druze wa Majdal Shams liliulenga uwanja wa mpira na kuwaua vijana wenye umri kati ya miaka 10 hadi 20.

Israel yalilaumu kundi la Hezbollah kwa shambulizi katika eneo la milima ya Golan

Israel imelilaumu kundi la Hezbollah la Lebanon linaloungwa mkono na Iran kwa ufyatuaji wa kombora hilo lakini kundi hilo limesema halikuhusika.

Netanyahu asema Hezbollah italipia vikali

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Israel lazima ichukuwe hatua kali kuhusiana na tukio hilo na kwamba Hezbollah italipia vikali.

Iran yaionya Israel dhidi ya hatua za kijeshi kuelekea Lebanon

Hata hivyo Iran imeionya Israel kwamba matukio mapya ya kijeshi nchini Lebanon yanaweza kusababisha matokeo yasiyotarajiwa.

Serikali ya Lebanon imetoa wito wa kusitishwa mara moja kwa uhasama kutoka pande zote.