Vifaru vya kijeshi vya Israel vyaendeleza mashambulizi Rafah
29 Mei 2024Matangazo
Israel imeendeleza mashambulizi hayo leo baada ya Marekani kusema hatua zinazochukuliwa na Israel hazijafikia operesheni kubwa za kijeshi katika mji huo.Marekani iliitahadharisha Israel kuepuka kufanya mashambulizi makubwa.
Jana ni mara ya kwanza Israel kupeleka vifaru katikati ya mji wa Rafah licha ya mahakama ya Kimataifa inayosimamia haki,iliyoko nchini Uholanzi kuitaka isitishe mashambulizi kwenye mji huo.
Israel kuendeleza vita Gaza hadi mwishoni mwa mwaka 2024
Wakaazi wa Rafah wamesema vifaru hivyo vya kijeshi vya Israel viliingia hadi magharibi mwa mji huo kabla ya kuelekea kwenye eneo la usalama lililowekwa lililoko katika mpaka na Misri.