1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Vifaru vya Israel vyazidi kusogea kaskazini mwa Gaza

28 Oktoba 2024

Vifaru vya kijeshi vya Israel vimezidi kusogea katika miji ya kaskazini mwa Gaza na kwenye kambi ya kihistoria ya wakimbizi katika ukanda huo ambako raia takriban 100,000 wamenasa.

https://p.dw.com/p/4mJqY
Gaza | Khan Younis | Vifaru vya Israel
Vifaru vya IDF vikiwa na askari wenye silaha, wakati wakiendeleza kutoka angani na ardhini huko Khan Yunis, Gaza mnamo Machi 7, 2024.Picha: Mostafa Alkharouf/Anadolu/picture alliance

Shirika la huduma za dharura la Kipalestina ambalo limesema watu hao wamekwama katika miji ya Jabalia, Beit Lahiya na Beit Hanoun wakiwa hawana msaada wa matibabu wala chakula.

Shirika la habari la  Reuters halikuweza kuthibitisha juu ya idadi hiyo iliyotajwa.

Jeshi la Israel linasema, vifaru vyake viko kwenye eneo hilo kuendesha operesheni ya kuwasambaratisha wanamgambo wa Hamas wanaojipanga upya.

Madhila hayo ya Wapalestina yanaripotiwa wakati mazungumzo yanayoongozwa na Marekani, Misri na Qatar ya kutafuta makubaliano ya kusitisha vita yakiwa yameanza tena Jana Jumapili.

Rais wa Misri Abdel Fatah al-Sisi, amependekeza makubaliano ya mwanzo ya kusitisha vita kwa siku mbili, kutowa nafasi ya kuachiliwa mateka wa Israel na wafungwa wa Kipalestina.