Taka ambazo hazijakusanywa ni tatizo kubwa kwenye nchi zinazoendelea duniani, hasa Afrika na zinasababisha uchafuzi wa mazingira na magonjwa. Taarifa njema ni kwamba taka nyingi zinazotupwa Afrika zinaweza kutumika tena kutengezea bidhaa mpya. Kinachosikitisha, kiasi asilimia 10 tu ya taka zinazotupwa kila siku Afrika, ndiyo zinakusanywa.