1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVenezuela

Venezuela yawafunga waandanamaji kwenye jela za ulinzi mkali

1 Septemba 2024

Makundi ya haki za binaadamu nchini Venezuela yamesema zaidi ya watu 700 waliokamatwa wakati wa maandamano yaliyozuka baada ya uchaguzi wa rais unaozozaniwa wa taifa hilo wamehamishiwa kwenye magereza yenye ulinzi mkali.

https://p.dw.com/p/4k9C2
Uchaguzi wa Venezuela | kupingwa Nicolas Maduro
Wafuasi wa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro wakiandamana kusherehekea matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwezi uliopita, Caracas, Venezuela Agosti 28, 2024.Picha: Fausto Torrealba/REUTERS

Shirika huru lenye kujihusisha na uangalizi wa hali wafungwa "Venezuelan Prisons Observatory" limesema wafungwa hao waliokuwa wakishikiliwa katika vituo vya polisi kote nchini, wiki iliyopita walihamishiwa kwenye magereza mawili ya wafungwa sugu ambayo hapo awali yalikuwa yakidhibitiwa na magenge ya wahalifu.

Katika visa vingi uhamisho huo ulifanywa chini ya hali zenye kutiliwa mashaka, ambapo ndugu wa wafungwa hawakujulishwa kuhusu kuhamishwa kwena katika magereza hayo ya  Tocuyito na Tocoron.

Zaidi ya watu 2,400 walitiwa mbaroni kufuatia maandamano yaliyozuka baada ya Rais Nicolas Maduro kutangazwa mshindi wa uchaguzi tata wa Julai 28.