Vatikani yakasirishwa na mwenendo wa shirika la kitawa
20 Aprili 2012Kulingana na ripoti ya Vatikani, Shirika hilo limejiingiza katika kufuru kubwa ya imani yao kwa kuunga mkono utoaji mimba na utanasia yaani kifo cha huruma kwa mgonjwa aliyeteseka kwa muda mrefu.
Pia shirika linadaiwa kutoa maelekezo kinyume na misimamo ya maaskofu ambao ndiyo wenye mamlaka ya kutoa maelekezo ya kanisa katika majimbo yao.
Network waliunga mkono mswada wa Afya wa Rais Obama
Likitakiwa kufuata utaratibu wa sala na ibada za kanisa Katoliki, Vatikani imeamua kupitia upya muuongozo wa taasisi hii yenye watawa wa kike zaidi ya 57,000, ambayo hapo awali ilikuwa ikitoa mafunzo ya utawala na haki.
Usimamizi wote wa shirika hili la kitawa umewekwa chini ya Askofu Mkuu Peter Sartan kwa kipindi cha miaka mitano kutoka huko Marekani.
Shirika hilo kwa sehemu kubwa lilishiriki kuunga mkono mswada wa Afya wa Rais Baraka Oboma ambao baadae ukaja kuwa sheria ukiunga mkono utoaji mimba.
Sista Simone Campbell ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo amekirii kuwa ushiriki wao kwa karibu katka mswaada wa Afya wa Rais Oboma ndiyo umesababisha Vatikani kufikia maamuzi hayo.
Mswaada huo ulianza mwaka 2009 hadi 2010 na miezi michache baadae ukawa sheria lakini ripoti hiyo ya vatikani haikumtaja kabisa Rais Obama.
Sista Campbell anasema nafasi yao katika kuunga mkono mswaada huo inatokana kwa kuutazama mswaada huo kwa jicho ambalo ni kinyume na mtazamo wa maskofu wa Kanisa katoliki.
Mara baada ya Vatikani kutangaza kufanywa kwa uchunguzi juu ya shirika hili lenye watawa wengi wa kike, huku wakiwa na hospitali na wakifundisha watu kadhaa imani hiyo, iliwavunja moyo waliokuwa wanaliunga mkono. Kwa muda sasa watawa wa kike wa Marekani wakiwa na misimamo tofauti na Vatikani.
Taasisi hii ilikiuka mafunzo ya kikristo
Hali ya mashaka juu ya watawa wa kike nchini Marekani kulifanya Vatikani kuamua kufanywa kwa uchunguzi juu ya maisha yao katika makazi yao mpaka sasa taarifa ya uchunguzi ya hilo haijatolewa hadharani.
Kulingana na taarifa miongoni mwa waliofanya uchunguzi juu ya shirika hili sista Laurie Brink ambaye ni Profesa katika Chuo Kikuu cha Chicago huko Marekani, amesema shirika hili lilikuwa likivuka mipaka ya Ukristo na kuvuka hata kile Yesu alichofundisha.
Mkusanyiko huo wa Vatikani ulilopokea ripoti hiyo umesema walipokea barua kadhaa ambazo zilikuwa zinapinga msimamo wa Kanisa juu ya namna ya kujamiana na huku wakipinga utaratibu wa sakramenti ndani ya kanisa.
Maswali kadhaa yakiibuliwa na watawa hao juu ya utanasia na utoaji wa mimba. Lakini haya yanapigwa na Nick Cafardi ambaye amewahi kuwa mlezi wa wanafunzi katika shule ya Sheria ya Duquene akisema ripoti hiyo haionyeshi hali halisi ya misimamo ya watawa wa kike katika kanisa katoliki, Kwani Cafardi aliwahi kufanya kazi na watawa kwa muda mrefu,
Mwanasheria huyo ni miongoni mwa watu wanaomuunga mkono Rais Obama. Sifahamu kitu juu ya wachamungu bali nimeona mengi ndani ya nyumba za watawa wa kike zaidi ya niliyowahi kuyaona mahakamani, alimalizia mwanasheria huyo.
Mwandishi:Adeladius Makwega/APE
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman