Vatican yafananisha kubadilisha jinsia na kutoa mimba
9 Aprili 2024Matangazo
Kanisa hilo lilisema siku ya Jumatatu (Aprili 8) kuwa mambo yanakinzana na matakwa ya Mungu kwenye maisha ya mwanaadamu.
Tamko hilo la Vatican lenye kurasa 20 lililotolewa baada ya mapitio ya zaidi ya miaka mitano na kuthibitishwa na Mkuu wa Kanisa hilo, Papa Francis, tarehe 25 Machi na kisha kuagiza kuwa lichapishwe na kusambazwa.
Soma zaidi: (SW): Vatican yafanani... Vatican yaendelea kupinga kubadilisha jinsia
Kwa kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki, ambaye alikuwa anachukuliwa kama mwenye msimamo wa wastani na anayefanya juhudi kubwa ya kuwafikia watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, tamko hili lilipokelewa na jamii hiyo kama pigo kubwa.