Uwindaji faru Afrika Kusini waongezeka 2023
27 Februari 2024Matangazo
Afrika Kusini inahifadhi takriban nusu ya faru weusi barani Afrika, ambayo pia ina idadi kubwa ya faru weupe walio katika hatari kubwa ya kutoweka.
Faru wamekuwa wakiwindwa kutokana na pembe zao, zinazotumika kwenye nchi za mashariki mwa bara la Asia kwa kutengeneza dawa za kienyeji na vito.
Soma pia: Ndovu barani Afrika waathirika na uwindaji haramu
Waziri wa Mazingira wa Afrika Kusini Barbara Creecy amesema mwaka 2023 faru 406 waliuwawa katika mbuga za wanyama za serikali na wengine 93 katika mbuga na mashamba binafsi.
Ameongeza kuwa simba 307 pia waliwindwa katika mbuga ya wanyama ya Hluhluwe-Imfolozi iliyopo katika mkoa wa mashariki wa KwaZulu-Natal.