1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaUturuki

Uturuki yawakumbuka maelfu waliokufa tetemeko la 2023

6 Februari 2024

Mamilioni ya watu nchini Uturuki leo wamefanya kumbukumbu ya kuomboleza msiba uliotokana na tetemeko kubwa la Ardhi mwaka mmoja uliopita lililopiga nchini humo.Zaidi ya watu 53,000 waliuwawa kwenye janga hilo.

https://p.dw.com/p/4c5dG
Uturuki, Hatay | Mwaka mmoja baada ya tetemeko la mwaka 2023
Hadi leo uharibifu uliotokana na tetemeko hilo bado unashuhudiwa kwenye miji ya Uturuki.Picha: Efekan Akyuz/Middle East Images/AFP via Getty Images

Katika kumbukumbu ya kuadhimisha kile walichokiita "Janga la Karne," serikali imeandaa matukio mbalimbali ya kuwaenzi waliopoteza maisha kusini mwa Uturuki.

Katika mji mkuu wa mkoa wa kusini wa Hatay, Antakya, umati wa watu ulikabiliana na polisi wakati wa maadhimisho hayo. Watu waliimba nyimbo za kumtaka meya wa mji huo Luftu Savas ajiuzulu huku waziri wa afya Fahrettin Koca akizomewa wakati alipokuwa akitoa hotuba.

Mkoa wa Hatay ulioko kati ya  bahari ya Mediterania na mpaka wa Syria, ndio ulioathirika zaidi na tetemeko hilo la ardhi la ukubwa wa 7.8 katika kipimo cha richta.

Tetemeko hilo lilisababisha vifo vya zaidi ya watu 59,000.