Uturuki yawakamata watu 15 waliowashambulia Wamarekani
3 Septemba 2024Uturukiimewakamata wanachama 15 wa vuguvugu la kizalendo la vijana linalotuhumiwa kwa kuwashambulia na kuwapiga maafisa wa jeshi la wanamaji la Marekani katika mji wa magharibi wa Izmir. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na maafisa.
Waliokamatwa ni wanachama wa kundi linaloipinga sana Marekani la Turkish Youth Union, TGB, ambalo wanachama wake wamewahi kufanya mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa jeshi la wanamaji la Marekani.
Mabaharia hao ni sehemu ya wafanyakazi wa meli ya kivita ya Marekani USS Wasp ambayo imetia nanga Izmir tangu Septemba mosi.
Vuguvugu la TGB limedai kuhusika na shambulizi hilo likisema wanajeshi wa Marekani wenye damu ya wanajeshi wao na damu ya maalfu ya Wapalestina mikononi mwao hawawezi kuinajisi nchi yao. Tukio hilo limewaghadhabisha wengi nchini Uturuki.