1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki yaiwekea Israel vikwazo vya kibiashara

9 Aprili 2024

Uturuki imeiwekea vikwazo vya kibiashara Israel kuanzia kutokana na vita vyake huko Gaza katika bidhaa mbali mbali ikiwemo simiti, vyuma na vifaa vya ujenzi.

https://p.dw.com/p/4eZrq
Recep Tayyip Erdogan
Waziri wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan Picha: Omer Urer/Anadolu/picture alliance

Hatua hii mpya inajiri siku moja baada ya Uturuki kusema kuwa Israel imezuia jaribio lake la kudondosha misaada kwa Gaza. Awali Waziri wa Mambo ya Nje Hakan Fidan aliapa kulipiza kisasi dhidi ya Israel

"Hakuna kisingizio kwa Israel kuzuia jaribio letu la kupeleka misaada kwa ndege kwa watu wenye njaa Gaza. Kwa kukabiliwa na hali hii, tuliamua kuchukua mfululizo wa hatua mpya dhidi ya Israeli. Hatua zilizoidhinishwa na rais wetu, zitatekelezwa hatua kwa hatua, bila kuchelewa."

Kupitia mtandao wa kijamii wizara ya biashara ya Uturuki imesema, uamuzi huo utatekelezwa hadi Israel itakapotangaza kusitisha mapigano na kuruhusu usambazaji wa kutosha na usiokatizwa wa misaada ya kibinadamu Gaza.