1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Erdogan aapa kuendeleza mapambano na wapiganaji wa Kikurdi

12 Agosti 2015

Rais Recep Tayyip Erdogan amesema, Uturuki inaazimia kusonga mbele kwa moyo mmoja na kampeni ya kupambana na wapiganaji wa kikrudi mpaka alichoita gaidi wa mwisho amemalizika

https://p.dw.com/p/1GDrb
Türkei Malatya Polizei Anti PKK DHKP-C Aktion Verhaftung
Picha: picture-alliance/AA/N. Boskut

Erdogan amesema hayo wakati ndege za Uturuki zimefanya mashambulio mengine dhidi ya waasi wa kikurdi. Abdu Mtullya na tarifa zaidi.

Uturuki kwa sasa inapigana na pande mbili wakati mmoja- inapambana na magaidi wanaoitwa dola la kiislamu nchini Syria na wapiganaki wa Kikurdi kaskazini mwa Iraq na kusini mashariki, baada ya mashambulo kadhaa.

Lakini mpaka sasa mashambulio ya ndege ya Uturuki yamekuwa yanawalenga zaidi waasi wa kikurdi wa PKK ambao wamjibu kwa kuyakiuka makubaliano ya kusimamisha mapigano yaliyofikiwa mnamo mwaka wa 2013 na badala yake kuanzisha tena mashambulio makubwa hidi ya majeshi ya serikali ya Uturuki.

Tayyip Erdogan Türkei Porträt Stimmung neutral
Waziri Mkuu wa Uturuki Tayyip ErdoganPicha: Getty Images/F. Senna

Alizungumza kwa njia ya televisheni Rais wa Uturuki Erdogan alisema Uturuki itaendelea na mapamabano mpaka pale waasi watakapoziweka chini silaha zao

Tutasonga mbele na mapigano hadi silaha zitakapowekwa chini na hakuna gaidi hata mmpja atakaebakia ndani ya mipaka yetu.Na mimi sizungumzii juu ya sisi kuweka chini silaha bali nazungumzia juu ya kuwamaliza magaidi"

Ndege za Uturuki zilifanya mashambulio mengine usiku wa jana kuwalenga waasi wa kikurdi, baada ya waasi hao kufanya mashambulio na kuwaua askari sita wa jeshi la Uturuki.

Sehemu 17 za waasi wa kikurdi wa PKK zilipigwa na ndege za Uturuki, katika jimbo la Hakkari la kusini mashariki mwa Uturuki. Msemaji wa jeshi la Uturuki amearif kwamba vituo hivyo vyote 17 viliteketezwa.

Türkei Incirlik Air Base U.S. Air Force F-16
Ndege za kivita za Marekani katika kambi ya kijeshi ya Incirlik, UturukiPicha: Reuters/U.S. Air Force

Hapo juzi polisi wanne wa Uturuki waliuawa kutokana na shambulio la bomu lililotegwa barabarani katika jimbo hilo kusini mashariki, na mwanajeshi mmoja pia aliuawa baada ya helikopta kupigwa na kombora.

Katika kadhia nyingine afisa mmoja mwandamizi wa polisi aliuawa mjini Istanbul katika shambulio la kujitoa mhanga.

Waasi wa PKK wamedai kuhusika na shambulio hilo na wamethibitisha kwamna wapiganaji wao watatu waliuawa, ikiwa pamoja na mshambuliaji wao wa kujitoa mhanga. Waasi hao pia wamekanusha madai kwamba kikundi kimoja kinachofuata nasaha za Karl Marx kilihusika na shambulio hilo lililofanyika alfajiri mjini Istanbul.

Askari mwengine wa Uturuki aliuliwa jana usiku baada ya kushambuliwa kwa bunduki kwenye kituo cha kijeshi kilichopo katika mji wa Sirnak kusini mashariki mwa Uturuki.Uturuki imedai waasi wa kikurdi wanahusika na mauaji hayo.

Jeshi la Uturuki limearifu kwamba ndege zake mbili aina ya F-16 zilifanya mashambulio na kuziteketeza sehemu 17 za waaasi wa PKK katika jimbo hilo la kusini mashariki.

Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la habari la AFP askari wapatao 30 wa Uturuki wameshauawa tokea kuanza tena kwa mapigano baina ya waasi na majeshi ya Uturuki.

Mwandishi:Mtullya abdu.afpe,ZA
Mhariri:Josephat Charo