Sheria na HakiUturuki
Uturuki kujiunga kesi ya mauaji ya kimbari dhidi ya Israel
7 Agosti 2024Matangazo
Mashtaka hayo yaliwasilishwa na Afrika Kusini. Uturuki ni miongoni mwa nchi zilizojiunga hivi karibuni ili kushiriki katika kesi hiyo.
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan mara kwa mara ametoa miito ya kutaka Israel iadhibiwe na mahakama za kimataifa na amezikosoa nchi za Magharibi kwa kuiunga mkono Israel.
Mnamo mwezi wa Mei Uturuki ilisimamisha shughuli za kibiashara na Israel.
Afrika Kusini iliwasilisha kesi hiyo kwenye Mahakama ya Haki ya Umoja wa Mataifa, ICJ mwaka uliopita kwa kuilaumu Israel kwa kukiuka mkataba wa kuzuia mauaji ya halaiki, kutokana na operesheni zake za kijeshi kwenye Ukanda wa Gaza.
Hata hivyo, Israel imeyakanusha vikali madai hayo.