1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiUlaya

Uturuki kuchunguza kifo cha raia wake Ukingo wa Magharibi

13 Septemba 2024

Uturuki imeanzisha uchunguzi wake yenyewe kuhusu kisa cha kuuawa kwa mwanaharakati mwenye uraia wa Marekani na Uturuki. Mwanaharakati huyo aliuawa kwenye Ukingo wa Magharibi wiki iliyopita kwa kupigwa risasi.

https://p.dw.com/p/4kcAO
Ankara, Uturuki | Rais Tayyip Erdogan akiwa ameambatana na maafisa wengine wa ngazi za juu.
Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan akiwa ameambatana na maafisa wengine wa ngazi za juu.Picha: Emin Sansar/Anadolu/picture alliance

Mkasa huo ulitokea wakati wa maandamano ya kupinga makaazi ya Israel katika Ukingo huo.

Maafisa wa Israel walikiri kwamba risasi ya vikosi vyao ilimpiga lakini bila ya kukusudia. Marekani na Umoja wa Mataifa walilaani tukio hilo na kutaka uchunguzi ufanywe.

Mapema leo, wakati mwili wa marehemu ulipowasili Uturuki, Waziri wa Sheria wa Uturuki, Yilmaz Tunc, alisema wameanzisha uchunguzi kubaini waliohusika na kifo cha Aysenur Ezgi Eygi. 

Soma pia:Vitendo vya kandamizaji vyaongezeka Ukingo wa Magharibi

Hayo ni kulingana na shirika la Habari linalomilikiwa na serikali ya taifa hilo Anadolu. Waziri Tunc ameongeza kuwa Uturuki inapania kusihinikiza polisi ya kimataifa itoe waranti wa kukamatwa kwa wahusika wa mauaji hayo.