1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJapan

Utiririshaji maji ya Fukushima wapingwa Korea Kusini

8 Julai 2023

Mamia ya watu walikusanyika leo kwenye mji mkuu wa Korea Kusini, Seoul, kuishinikiza Japan kuufuta mpango wa kutitirisha baharini, maji kutoka kinu cha nyuklia cha Fukushima kilichoharibiwa naTsunami mwaka 2011.

https://p.dw.com/p/4Tcf7
Japan Okuma | Kernkraftwerk | Lagertanks für kontaminiertes Wasser
Maji yaliyohifadhiwa kutoka kinu cha Fukushima Picha: Philip Fong/AFP/Getty Images

Maandamano hayo yamefanyika siku moja baada ya serikali ya nchi hiyo kuidhinisha rasmi mpango huo wa Japan ikisema viwango vya mionzi kwenye maji yatakayoingizwa baharini kutoka kinu cha Fukushima ni salama.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti nishati ya nyuklia tayari liliridhia mpango huo wiki iliyopita likisema utiririshaji maji hayo yaliyosafishwa ili kuondoa karibu aina zote za mionzi utazingatia viwango vya kimataifa. Licha ya hayo waandamanaji mjini Seoul walibeba mabango yenye ujumbe wa kuonesha upinzani wa mpango huo.

Kiasi cha mita za ujazo milioni 1.33 za maji yaliyotumika kupooza mitambo yamekusanyika katika eneo la Fukushima, yakisubiri kumwagwa baharini ndani ya kipindi cha miongo kadhaa inayokuja.