1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utekaji nyara unatumika kuukandamiza upinzani Burkina Faso

27 Februari 2024

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch limesema utawala wa kijeshi Burkina Faso unatumia utekaji nyara kunyamazisha upinzani

https://p.dw.com/p/4cxVQ
Burkina Faso Demonstrant mit Flagge Russland
Picha: ISSOUF SANOGO/AFP/Getty Images

Tangu mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka 2023, wanaume wasiojulikana wamewateka nyara wanaharakati sita na wanachama wa upinzani katika mji mkuu wa Ouagadougou, na kuzidisha wasiwasi wa watu kutoweka ghafla.

Human Rights Watch imesema utawala wa Burkina Faso unapaswa kuchukua mikakati madhubuti ya kuwapata wale ambao hawajulikani waliko na kuwawajibisha wale wanaohusika na uhalifu huo.