SiasaMyanmar
Utawala wa kijeshi wa Myanmar warefusha muda hali ya dharura
31 Julai 2023Matangazo
Tangazo hilo limetolewa na Kaimu Rais Myint Swe mbele ya Baraza Tawala la Kijeshi ambapo amesema hali ya hatari iliyodumu kwa zaidi ya miaka miwili itarefushwa kwa kipindi kingine cha nusu mwaka kuanzia Agosti Mosi.
Soma zaidi: Myanamar: Jeshi limetangaza hali ya dharura na kuchukua madaraka
Jeshi la Myanmar lapinga cheo kipya cha Su Kyi
Sababu iliyotolewa ni kuendelea kwa mapigano kwenye mikoa kadhaa ya nchi hiyo na kwamba utawala wa kijeshi unahitaji muda zaidi kurejesha utulivu kabla ya kuondoa tangazo la hali ya dharura na kuitisha uchaguzi.
Myanmar imetumbukia kwenye mzozo mkubwa kisiasa tangu jeshi lilipompindua kiongozi wa kiraia, Aung San Suu Kyi, mwaka 2021 na kutekeleza hatua kadha za kukandamiza wakosoaji wake.