1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Myanmar: Yaongeza muda wa hali ya dharura kwa miezi sita

31 Julai 2024

Utawala wa kijeshi wa Myanmar unaokabiliwa na shinikizo, umeongeza muda wa hali ya hatari kwa miezi sita huku jeshi hilo likijitahidi kudumisha utawala wake

https://p.dw.com/p/4ixA6
Myanmar | Min Aung Hlaing
Kiongozi wa kijeshi wa Mnyamar Jenerali Aung HlaingPicha: Aung Shine Oo/AP Photo/picture alliance

Hayo yanajiri wakati mapigano yakizuka katika maeneo kadhaa nchini Myanmar na hali ya uchumi ikidorora.

Kituo cha televisheni cha Myawaddy kinachoendeshwa na jeshi hilo, kimesema kuwa Baraza la Usalama na Ulinzi wa Taifa, liliamua kuongeza muda wa sheria hiyo ya hali ya dharura ili kutoa muda zaidi wa kuweka pamoja data ya idadi ya watu kwenye orodha za wapigakura. 

Maandamano yaendelea Mnyanmar kushinikiza utawala wa kiraia

Utawala huo wa kijeshi umesema utafanya uchaguzi mwaka ujao.