Uswisi yazuia mali za Ben Ali
20 Januari 2011Waziri wa Mambo ya Nje wa Uswisi, Micheline Calmy-Rey amesema anataka kuzuia matumizi yoyote mabaya ya fedha za umma.
Wakati huo huo, Benki Kuu ya Tunisia imeichukua taasisi ya kifedha iliyokuwa inadhibitiwa na mkwe wa Ben Ali.
Mapema, viongozi wa Tunisia walisema pia watachunguza mali za Ben Ali zilizopo nje ya nchi zikiwemo akaunti za benki na nyumba.
Imeripotiwa kuwa Ben Ali aliyekimbilia Saudi Arabia Ijumaa iliyopita aliondoka nchini Tunisia na tani 1.5 za madini ya dhahabu.
Kwa upande mwingine, karibu waandamanaji 2,000 katika mji mkuu wa Tunis wanadai kufukuzwa kwa mawaziri wote ambao wanahusishwa na Ben Ali katika serikali mpya ya muungano.
Na taarifa nyingine zinaeleza kuwa viongozi wa serikali hiyo ya mpito wamewaachilia huru wafungwa wa mwisho wa kisiasa.