1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Uswisi kuandaa mkutano wa amani ili kumaliza vita Ukraine

16 Januari 2024

Serikali ya Uswisi imeridhia ombi la rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky la kuandaa mkutano wa amani wa viongozi wa dunia utakaokuwa na dhima ya kukomesha uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4bHmj
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alipowasili nchini Uswisi siku ya Jumatatu.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alipowasili nchini Uswisi siku ya Jumatatu.Picha: ALESSANDRO DELLA VALLE/AFP/Getty Images

Hayo yameelezwa na rais Zelensky aliye ziarani nchini Uswisi kusaka uungaji mkono zaidi wa kimataifa katika vita baina ya nchi yake na Urusi.

Akizungumza na waandishi habari baada ya mazungumzo na rais wa Uswisi, Viola Amherd, Zelensky amesema mataifa hayo mawili yataanza kazi mara moja kutayarisha mkutano huo nchini Uswisi ambao hata hivyo hautaialika Urusi.

Amesema mkutano huo wa ngazi ya viongozi wakuu wa mataifa utatafuta njia ya kumaliza vita chini ya misingi haki na inayorejesha heshima na utii wa sheria za kimataifa.

Baadae hii leo kiongozi hiyo ataelekea mjini Davos, Uswisi kuhudhuria kongamano la kila mwaka la uchumi duniani.