1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Usalama-Liberia

12 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFst
Monrovia: Hali nchini Liberia inaelezwa kuwa ni shwari kidogo , baada ya kutiwa nguvuni wanajeshi 37 wa serikali ya zamani, ambao wamekua wakiendesha vitendo vya vitisho dhidi ya raia na uporaji maduka katika mji mkuu-Monrovia. Wanajeshi hao walidai kukasirishwa na hatua ya serikali mpya kutangaza amri ya kutotoka nje usiku. Msemaji wa shughuli za amani za umoja wa mataifa nchini Liberia, amesema hata hivyo kwamba bado nchi hiyo haiko kwenye utulivu na hali za binaadamu ni mbaya- huku mashirika ya kibinaadamu yakishindwa kutuma misaada nje ya mji mkuu Monrovia.