1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Urusi yazuia mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani

31 Agosti 2023

Maafisa wa Urusi wamesema wamezuia mashambulizi mapya ya Ukraine siku moja baada ya ndege zisizokuwa na rubani za Ukraine kufanya mashambulizi katika maeneo ya magharibi mwa Urusi.

https://p.dw.com/p/4VmGF
Mwanajeshi wa Ukraine akiandaa ndege isiyokuwa na rubani
Mwanajeshi wa Ukraine akiandaa ndege isiyokuwa na rubani Picha: Wolfgang Schwan/AA/picture alliance

Moja kati ya shambulio hilo la ndege zisizokuwa na rubani, lililolenga uwanja wa ndege mbali na mipaka ya Ukraine, iliharibu ndege za kijeshi za Urusi.

Mkuu wa mkoa wa Crimea, uliokuwa sehemu ya Ukraine na baadaye kuchukuliwa na Urusi mwaka 2014, ameeleza kuwa mashambulizi ya makombora ya Ukraine yamezuiwa.

Mnamo siku ya Jumanne, maafisa wa Urusi walithibitisha kutokea kwa kwa mashambulizi katika mji wa Bryansk na maeneo mengine matano, ikiwemo Moscow.

Wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema waliohusika na mashambulizi hayo wataadhibiwa na kuongeza kuwa, mashambulizi hayo ya ndege zisizokuwa na rubani hayangefika mbali bila ya msaada wa mataifa ya magharibi.