MigogoroUrusi
Urusi yawaondoa watoto kutoka Belgorod mpakani na Ukraine
10 Januari 2024Matangazo
Hayo yamesemwa na gavana wa eneo hilo, Vyacheslav Gladkov. Wakazi wapatao 300 walikuwa tayari wameondoka Belgorod, katika operesheni kubwa ya kuwahamisha watu kutoka mji mkubwa wa Urusi tangu nchi hiyo ilipoanza uvamizi wake dhidi ya Ukraine mnamo Februari 2022.
Soma pia: Urusi: Ukraine yashambulia tena Belgorod kwa makombora-droni
Kundi la kwanza la watoto wameondoka Belgorod kuelekea eneo jirani la Voronezh, ambalo liko mbali na mpakani. Gavana Gladkov ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Telegram kwamba watoto 93 wa darasa la kwanza hadi la nne kutoka shule mbalimbali katika mji wa Belgorod watapumzika na kuangaliwa afya zao katika kambi za afya za watoto.