1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yavishtumu vyombo vya habari vya Marekani

20 Agosti 2024

Urusi imemuita afisa mmoja mkuu wa Marekani juu ya ripoti katika vyombo vya habari vya Marekani kutoka sehemu ya eneo lake la Kursk na kuonya itawachunguza waandishi habari kwa kuvuka mpaka wake kinyume cha sheria.

https://p.dw.com/p/4jhgk
Vikosi vya Ukraine vimevamia eneo la mpaka la Kursk katika ardhi ya Urusi mnamo Agosti 16,2024
Eneo la mpakani kati ya Urusi na Ukraine la Sudzha lililoharibiwaPicha: Chubotin Kirill/Ukrinform/ABACA/IMAGO

Urusi imevishutumu vikali baadhi ya vyombo vya habari vya Magharibi kwa kuripoti kutoka eneo linalodhibitiwa na vikosi vya Ukraine tangu uvamizi wake wa kushtukiza, na kuanzisha  uchunguzi wa uhalifu dhidi ya waandishi habari wa Italia kwa ripoti ya televisheni kutoka eneo hilo.

Urusi yamtaka afisa wa Marekani kulaani vitendo vya waandishi habari

Wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema ilimtaka Naibu Mkuu wa Ubalozi wa Marekani Stephanie Holmes kutangaza pingamizi kali kuhusiana na vitendo vya uchochezi vya waandishi habari wa Marekani ambao waliingia katika eneo hilo la Kursk kinyume cha sheria.

Soma pia:Zelensky: Wanajeshi wetu wanatimiza malengo yao huko Kursk

Wizara hiyo haikutaja shirika husika la habari lakini imesema inapanga hatua mwafaka za uchunguzi ili kuwachukulia hatua za kisheria waandishi hao.

Wizara hiyo ya mambo ya nje pia imesema vitendo kama hivyo vinaonyesha kuwa Marekani ni mshirika wa moja kwa moja katika mzozo kati ya Urusi na Ukraine, hoja ambayo Urusi imekuwa ikiitumia kwa muda mrefu kuionyesha Ukraine kama nchi ambayo haifanyi maamuzi yake yenyewe.

Vyombo kadhaa vya habari vya Marekani vimechapisha ripoti kutoka Sudzha

Katika siku za hivi karibuni, vyombo kadhaa vya habari vya Marekani vimechapisha ripoti kutoka ndani ya Sudzha, mji mkuu ambao umetekwa na Ukraine.

Zaidi ya watu 122,000 wameondoka katika maeneo ya mpaka ya Kursk

Wizara ya kukabiliana na hali za dharura ya Urusi imesema zaidi ya watu 122,000 wameondoka katika maeneo ya mpaka ya Kursk nchini Ukraine tangu uvamizi wa Ukraine katika eneo hilo.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akutana na waziri mkuu wa Uhispania Pedro Sánchez mjini Madrid , katika ziara yake ya kwanza rasmi nchini Ushispania mnamo Mei 27,2024
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Juan Carlos Rojas/picture alliance

Artem Sharov, mwakilishi wa wizara hiyo amesema kuwa katika eneo la Kursk, vitengo vya Wizara ya Hali ya Dharura ya Urusi vinaendelea kufanya kazi katika hali ya dharura na kwamba kazi inaendelea ya kuwapa makazi mapya wakaazi katika maeneo ya mipakani na kuwaeka katika maeneo salama.

Ukraine yaidhinisa muswada dhidi ya mashirika yenye uhusiano na Urusi

Katika hatua nyingine, wabunge nchini Ukraine wameidhinisha muswada unaoharamisha mashirika ya kidini yenye uhusiano na Urusi, likiwemo Kanisa la Orthodoks la Ukraine  linalohusishwa na Urusi.

Muswada huo ulipongezwa na ofisi ya Zelensky.

Soma pia:Zelensky asema aanajeshi wanazingatia sheria za kiutu wanapozidi kuingia Kursk

Katika ujumbe aliochapisha katika mtandao wa Telegram, mkuu wa watumishi katika ofisi hiyo Andriy Yermak, alisema kuwa hakutakuwa na kanisa la Urusi nchini Ukraine.

Nchini Urusi, msemaji wa wizara ya mambo ya nje Maria Zakharova, amesema Ukraine inajaribu kuharibu Uorthodoksi wa kweli.

Muswada unasubiri kutiwa saini na Rais kuwa sheria

Muswada huo unahitaji kutiwa saini na Rais Volodymyr Zelensky ili kuanza kutumika na utachukua miaka kutekelezwa, lakini bado ulisababisha hali ya wasiwasi miongoni mwa wafuasi wa Kanisa la Orthodoks la Ukraine.