1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yatangaza bajeti kubwa ya ulinzi kwa mwaka 2025

1 Desemba 2024

Rais wa Urusi Vladmir Putin ameidhinisha mipango ya bajeti ya nchi hiyo ambapo ameongeza kwa kiwango cha juu matumizi ya kijeshi ya mwaka 2025.

https://p.dw.com/p/4ncTG
Kasachstan | Gipfel Organisation der kollektive Sicherheit in Astana | PK Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin akiongea na vyombo vya habari huko Astana, Kazakhstan,Picha: Ramil Sitdikov/AP Photo/picture alliance

Asilimia 32.5 ya bajeti iliyochapishwa katika tovuti ya serikali imeelekezwa katika masuala ya ulinzi wa taifa ambazo ni sawa na zaidi ya dola bilioni 145. Bajeti hiyo ya ulinzi ya Urusi imeongezeka ikilinganishwa na ile ya mwaka huu ya asilimia 28.3. Bajeti hiyo ilipitishwa pia na bunge la Urusi,Duma na baraza la shirikisho. Hatua hiyo ya Urusi imechukuliwa wakati nchi hiyo ikitaka kuchukuwa ushindi wa vita ilivyovianzisha nchini Ukraine.Kutangazwa kwa bajeti hiyo ya Urusi kumekuja wakati pia rais mpya wa baraza la Ulaya Antonio Costa na mkuu wa sera za nje za Umoja huo Kaja Kallas wakiitembelea Ukraine kwa mara ya kwanza tangu walipochukua nafasi hizo mpya. Ziara ya viongozi hao inalega kutowa ujumbe thabiti wa kuiunga mkono Ukraine.