Urusi yashutumiwa kashambulia hospitali Ukraine
10 Julai 2024Wakati wa mkutano huo, afisa mmoja wa Umoja huo, alilaani shambulio hilo na kulitaja kama uhalifu wa kivita huku wafuasi wa Ukraine kwa mara nyingine tena wakishtumu uvamizi wa Urusi nchini humo. Mwakilishi wa Ufaransa, Nicolas de Rivière, aliutaja uvamizi huo wa Urusi kuwa suala jipya katika orodha ya uhalifu wa kivita ambapo Urusi inapaswa kuwajibishwa. China, mshirika wa Urusi, pia ilionyesha wasiwasi katika matamshi ambayo yanaweza kuonekana kama ishara kwa Moscow. Naibu balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Geng Shuang, amesema kwa bahati mbaya, mapigano nchini Ukraine yameongezeka na mara kwa mara kumekuwa na mashambulizi ya kikatili ambayo yamesababisha mauaji ya watu wengi. Hata hivyo China imedumisha uangalifu wake wa kawaida na haikumshtumu moja kwa moja mshirika wake wa karibu Urusi.