MigogoroSyria
Urusi yashambulia ngome mbili za wanamgambo nchini Syria
7 Oktoba 2024Matangazo
Jeshi la anga la Urusi limefanya mashambulizi katika ngome mbili za wanamgambo nchini Syria nje kidogo ya al-Tanf, ambayo ni kambi ya jeshi la Marekani.
Hayo ni kwa mujibu wa shirika la habari la Urusi RIA.
Soma pia: Mashambulizi ya Israel yaharibu barabara ya Lebanon-Syria
Shirika hilo la habari likimnukuu kiongozi wa kituo cha Urusi cha maridhiano ya pande zinazohasimiana nchini Syria Oleg Ignasyuk, hata hivyo halikuweka wazi eneo kulikofanyika mashambulizi hayo japo limeeleza kuwa wanamgambo hao wameondoka eneo la al-Tanf linalopakana na Jordan.