MigogoroUkraine
Urusi yashambulia maeneo mbalimbali nchini Ukraine
29 Machi 2024Matangazo
Mapema Ijumaa, Gavana wa mkoa wa Dnipro Serhiy Lysak amesema mtu mmoja amejeruhiwa na miundombinu kadhaa ilishambuliwa katika wilaya ya Kamianske.
Mashambulizi mengine yameripotiwa mashariki mwa Ukraine ambako mapigano makali yameshuhudiwa karibu na miji iliyoharibiwa vibaya na vita ya Avdiivka na Bakhmut. Kamandi kuu ya jeshi la Kiev imesema jumla ya sehemu 48 huko Kharkiv zimeshuhudia mapigano makali.
Soma pia: Ukraine kuimarisha ulinzi kufuatia ongezeko la mashambulizi ya Urusi
Hayo yanajiri wakati Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amezungumza kwa njia ya simu na Spika wa Bunge la Marekani Mike Johnson na amemueleza umuhimu wa kupokea msaada wa kijeshi uliozuiliwa wa dola bilioni 60 ili kukabiliana na uvamizi wa Urusi.