Vikosi vya Urusi vinaudhibiti wa mji wa Kurakhove wa Ukraine
6 Januari 2025Matangazo
Mji huo wa Kurakhove ni kituo cha kutoa msaada wa vifaa kwa vikosi vya Ukraine na Urusi imesema kulikamata eneo hilo kumeathiri upatikanaji wa vifaa na msaada wa kiufundi kwa vikosi vya Ukraine.Katika hatua nyingine, jeshi la anga la Ukraine limesema leo Jumatatu kwamba imeyadungua makombora mawili chapa KH-59 yaliyorushwa na Urusi usiku wa kuamkia leo. Hapo jana Ukraine ilisema kwamba vikosi vyake vimeanzisha mashambulizi mapya ya kijeshi katika mji wa magharibi wa Urusi wa Kursk ikiwa ni muendelezo wa mashambulizi yake ya kushtukiza katika eneo hilo tangu wakati wa majira ya joto mwaka jana.