1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yasema mazungumzo ya DAVOS hayatafanikiwa

15 Januari 2024

Urusi imesema Jumatatu kuwa mazungumzo ya Davos kuhusu mapendekezo ya amani nchini Ukraine hayatafanikiwa kwa sababu Moscow haishiriki katika majadiliano hayo.

https://p.dw.com/p/4bGIq
Msemaji wa serikali ya Urusi, Dmitry Peskov
Msemaji wa serikali ya Urusi, Dmitry PeskovPicha: Mikhail Tereshchenko/TASS/dpa/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na viongozi muhimu wa Mashariki ya Kati wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo wa jukwaa la kiuchumi Duniani wiki hii, ukiyaweka mazungumzo ya kumaliza vita vya Gaza na Ukraine kileleni mwa mada zitakazojadiliwa na viongozi mashuhuri wa ulimwengu. Msemaji wa Ikulu ya Urusi - Kremlin, Dmitry Peskov amesema:

"Tumerudia mara kwa mara tathmini yetu ya mchakato huu wa amani ya Ukraine. Kimsingi, hii ni kama kuzungumza kwa ajili ya kuzungumza tu, ni mchakato ambao sio na hauwezi kuwa na lengo la kufikia matokeo yoyote maalum kwa sababu rahisi na ya wazi - hatushiriki katika hilo. Na bila ushiriki wetu, bila shaka, majadiliano yoyote yanawezekana, lakini hayana matarajio ya matokeo yoyote."

Mkutano wa Davos unafunguliwa rasmi kesho na utakamilika Ijumaa ukiwashirikisha wajumbe 2,800 wakiwemo wakuu 60 wa nchi na serikali.