Urusi yasema itajibu vikali mashambulizi dhidi yake
24 Mei 2023Onyo hilo limejiri baada ya ndege za kivita za Urusi na makombora kupambana na kundi lenye silaha lililovuka mpaka kutoka Ukraine.
Waziri wa Ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu amewaambia maafisa wa jeshi kwamba wataendelea kujibu mara moja vitendo kama hivyo vya wanamgambo wa Ukraine.
Aidha, msemaji wa Ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov amesema nchi hiyo haina nia ya kusitisha vita na Ukraine.
Wakati huo huo, Shirika la Afya Duniani, WHO leo limepitisha azimio kulaani uchokozi wa Urusi dhidi ya Ukraine, ikiwemo amshambulizi kwenye vituo vya afya.
Azimio hilo limepitishwa kwa kura 80 dhidi ya 9, huku nchi 52 zikijizuia na 36 hazikuhudhuria.
Azimio hilo lililowasilishwa na WHO katika mkutano wake wa mwaka, na pia limetaka kutathminiwa kwa athari za uvamizi wa Urusi kwenye sekta ya afya.