Urusi yasema imezuia jaribio la shambulizi Moscow
21 Agosti 2023Watu wasiopungua wawili walijeruhiwa na vifusi vya ndege hizo zilizodunguliwa.
Tukio hilo liliathiri safari za ndege katika viwanja vinne vya ndege vya mji huo kwa saa kadhaa. Takriban safari za ndege 50 kutoka na kuingia Moscow zilicheleweshwa.
Urusi imeilaumu Ukraine kwa kufanya mashambulizi hayo. Lakini Ukraine kwa kawaida huwa haitoi kauli yoyote kuhusu kuhusika kwake.
Hayo yakijiri, rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema Jumatatu kwamba ana imani Urusi itashindwa kwenye vita vya nchini Ukraine.
"Wajua nina uhakika tutashinda kwa sababu ukweli upo upande wetu na watu wetu wote pia. Kwa hivyo ninafikiri mwajua, tunasubiri wakati huo, na utakuwa ushindi wa ukweli, demokrasia, wa wat una wa mataifa. Ahsante sana kwa misaada yenu.”
Zelensky apongeza washirika kwa misaada ya silaha
Aliyasema hayo nchini Uholanzi kwenye hotuba yake nje ya bunge la taifa hilo, huku umati mkubwa wa watu uliojitokeza ukishangilia.
Zelensky alitoa kauli hiyo siku moja tu baada ya Uholanzi na Denmark kuipatia Ukraine ndege za kivita F-16, kwa lengo la kuimarisha nguvu yake ya angani dhidi ya mashambulizi ya vikosi vya Urusi.
Urusi tayari imetahadharisha leo Jumatatu kwamba kuipa Ukraine ndege hizo ni kuzidisha mgogoro.
Mnamo mwezi Julai, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov alisema serikali yake itachukulia hatua ya kuipa Ukraine ndege chapa F-16 kama kitisho cha nyuklia kwa sababu ya uwezo wa ndege hizo kubeba silaha za atomiki.
Vikosi vya Ukraine vyadai kukomboa sehemu ya Bakhmut
Katika tukio jingine, Ukraine imesema vikosi vyake vimekomboa sehemu ya mashariki mwa mji unaokumbwa na mapigano makali ya Bakhmut, lakini havijapata mafanikio makubwa eneo la kusini mwa mji huo.
Ripoti: Kiasi wanajeshi 500,000 wameuwawa au kujeruhiwa kwenye vita Ukraine
Naibu Waziri wa Ulinzi Ganna Malyar amesema hayo Jumatatu. Lakini Urusi imejibu ikisema vikosi vyake vinaimarisha ngome zao mashariki mwa Kharkiv na vimevisukuma mbali vikosi vya Ukraine mbali kusini mwa mji huo.
Ukraine ilianzisha operesheni ya kujibu mashambulizi ya vikosi vya Urusi mnamo mwezi Juni, baada ya kupokea silaha na zana Zaidi kutoka kwa washirika wake wan chi za Magharibi.
Kabla ya kuvamiwa na hatimaye kukamatwa na vikosi vya Urusi mwaka huu baada ya mapigano ya miezi kadhaa, mji wa kiviwanda wa Bakhmut ulikuwa na takriban wakaazi 70,000.
(Vyanzo: AFPE, RTRE)