1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yasema haiamini taarifa za Ukraine kuhusu mashambulizi

1 Machi 2023

Urusi imesema kwamba haiamini taarifa ya mshauri wa rais wa Ukraine Mykhailo Podolyak kwamba Ukraine hailengi maeneo ya Urusi kwa mashambulizi.

https://p.dw.com/p/4O7gq
Russland | Dmitri Peskow
Picha: Valery Sharifulin/TASS/dpa/picture alliance

Msemaji wa ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov ameyasema haya leo siku moja baada ya maafisa wa Urusi kuilaumu Ukraine kwa kujaribu kufanya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani.

Soma pia: Urusi yazidisha mashambulizi Bakhmut

Peskov amesema majaribio hayo ya mashambulizi ndio ya hivi karibuni kufanywa katika mipaka ya Urusi, mashambulizi ambayo Ukraine haijajitokeza hadharani kuthibitisha kuhusika.

Hayo yakiarifiwa, Ukraine imesema kwamba imepita kipindi kigumu cha mashambulizi ya Urusi katika miundo mbinu yake ya maji na nishati, wakati ilipoingia katika siku ya kwanza ya msimu wa machipuko.

Lakini katika mji wa mashariki wa Bakhmut, Ukraine iko kwenye shinikizo wakati ambapo Urusi imesema imezidungua ndege kadhaa zisizo na rubani katika rasi ya Crimea.