MigogoroUrusi
Urusi yapambana kuuzima moto kwenye ghala ya mafuta
20 Agosti 2024Matangazo
Moto huo umesababishwa na shambulio lililofanywa na ndege za droni za Uraine kwenye bohari ya mafuta katika mji wa Proletarsk.
Urusi imesema wazima moto kadhaa wamejeruhiwa. Wazima moto wapatao 520 wanapambana na moto huo ambao umezagaa kwenye eneo la kilometa za mraba 10,000.
Gavana wa Rostov Vasily Golubev amesema wazima moto 41 wanapata matibabu, huku wengine kadhaa wakiwa na majeraha ya moto.
Hakuna raia aliyeripotiwa kujeruhiwa.