SiasaUrusi
Urusi yaonyesha kutojali mustakabali wa OSCE
2 Desemba 2023Matangazo
Katika hotuba yake, waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema, hajali kuhusiana na mwelekeo wa shirika hilo kwa kuwa limekuwa kile alichokiita, kiambatisho cha jumuiya ya NATO na Umoja wa Ulaya.
Malta ndiyo nchi iliyochaguliwa kama mwenyekiti mpya na mwandalizi wa mkutano ujao mwakani, ambapo imeichukua nafasi ya Estonia ambayo ni mwanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO ambayo Urusi ilipinga nchi hiyo kupewa uenyekiti.
Lengo la shirika hilo ni mijadala ya masuala ya usalama ingawa Urusi imekuwa ikizuia maamuzi muhimu ya shirika hilo lenye wanachama 57.
Ukraine inaitaka OSCE iufutilie mbali uanachama wa Urusi la sivyo shirika hilo litasambaratika polepole.