1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaionya Magharibi kuhusu silaha za Ukraine

20 Septemba 2024

Urusi imesema hivi leo kuwa nchi za Magharibi zinapaswa kuacha kuipatia Ukraine silaha na kufadhili kile ilichokiita "shughuli za kigaidi", ikiwa zinayo nia ya dhati ya kukomesha vita hivyo.

https://p.dw.com/p/4ktNl
Rais Vladimir Putin wa Urusi.
Rais Vladimir Putin wa Urusi.Picha: Vyacheslav Prokofyev/Sputnik/REUTERS

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Urusi, Maria Zakharova, amewaambia waandishi wa habari kwamba mpango wa amani uliopendekezwa na Rais Volodymyr Zelenskiy wa Ukraine haukidhi vigezo vya kusuluhisha mzozo huo.

Soma zaidi: Rais Vladimir Putin asema wako tayari kwa mazungumzo na Ukraine, kwa kuzingatia makubaliano ya awali

Siku ya Jumatano (Septemba 18) Zelenskiy alisema Ukraine imekamilisha maandalizi ya mpango wa kuishinda Urusi ambao anakusudia kuujadili na Rais Joe Biden atakafanya ziara nchini Marekani wiki ijayo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Ryabkov, amesisitiza hii leo kuwa Marekani inapaswa kuzingatia onyo la Moscow juu ya hatari ya kutanuka kwa mzozo wa Ukraine.