1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Urusi yafanya mashambulizi ya usiku kucha nchini Ukraine

8 Novemba 2024

Urusi imefanya mashambulizi ya usiku kucha ya droni na makombora nchini Ukraine na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kuwajeruhi wengine zaidi ya 30 katikati, kusini, na kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4mmsT
Shambulizi la Urusi mjini Odesa Ukraine
Shambulizi la Urusi mjini Odesa UkrainePicha: Ministry for Communities and Territories Development of Ukraine via REUTERS

Urusi imefanya mashambulizi ya usiku kucha ya droni na makombora nchini Ukraine na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kuwajeruhi wengine zaidi ya 30 katikati, kusini, na kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Haya yamesemwa leo na maafisa wa Ukraine.

Jeshi la anga la Ukraine limesema vikosi vya Urusi vilirusha droni 92na makombora matano katika maeneo 12 ya nchi hiyo.

Droni 62 na makombora manne yalitunguliwa huku jeshi hilo likipoteza mwelekeo wa droni 26, ambazo linasema zina uwezekano kwamba zilitunguliwa kielektroniki.

Wizara ya ulinzi ya Ukraine imesema mtu mmoja alijeruhiwa katika eneo la Odesa ambapo miundo mbinu na makazi ya kiraia iliharibiwa na watu tisa kujeruhiwa.

Gavana wa eneo hilo Oleh Syniehubov pia amesema Urusi ilishambulia mji wa Kharkiv katika eneo la kaskazini mashariki kwa mabomu yakuongozwa.

Rais wa nchi hiyo Volodymyr Zelenskiy, ametoa ombi jipya kwa washirika wake kusaidia kuimarisha ulinzi wa anga wa nchi hiyo.