Urusi yafanya mashambulio makubwa Ukraine
25 Desemba 2024Katika mashambulio hayo mtambo wa kuzalisha umeme uliharibiwa. Asubuhi hii ya Krismasi, watu nchini Ukraine walilazimika kujificha kwenye vituo vya usafiri.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema Urusi ilifanya shambulio lisilo la kibinadamu kwa kurusha makombora na droni ili kuhujumu gridi ya nishati ya nchi yake.
Soma pia:Urusi yaushambulia mji wa Kryvyi Rih kusini-mashariki mwa Ukraine
Ukraine inakabiliwa na majira ya baridi kali zaidi kuwahi kutokea tangu kuanza vita miaka takriban mitatu iliyopita, wakati ambapo Urusi inaongeza mashambulizi yake ya anga huku wanajeshi wake wakisonga mbele mashariki mwa Ukraine.
Wakati huo huo, majeshi ya Urusi yanadai kuziteka sehemu zaidi ya 190 mnamo mwaka huu. Wizara ya ulinzi ya nchi hiyo pia imesema vikosi vyake vilidungua ndege 59 za Ukraine jana usiku.