1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi: Ukraine imehusika kushambulia eneo la Belgorod

22 Mei 2023

Urusi imesema Uvamizi uliofanywa na Ukraine katika eneo la mpakani mwa nchi yake la Belgorod ulilenga kuziondowa hisia kwenye hatua ya kunyakuliwa kwa mji wa Bakhmut, baada ya Moscow kudai kuukamata mji huo.

https://p.dw.com/p/4Rfz1
 Videokonferenz | Putin - Raisi
Picha: Mikhail Klimentyev/Kremlin/Sputnik/REUTERS

Maafisa wa Urusi wamesema kiasi watu sita walijeruhiwa kwenye shambulio lililofanyika leo Jumatatu. Hata hivyo Ukraine imekanusha kuhusika na uvamizi huo wa kulishambulia eneo hilo ambalo ni ardhi ya Urusi, baada ya Urusi kusema inapambana na kundi lililofanya hujuma hizo.

Soma pia: Kundi la Wagner ladai kuudhibiti mji wa Bakhmut

Mshauri wa rais wa Ukraine, Mikhaylo Podoyak amesema nchi hiyo inafuatilia matukio katika eneo hilo la Belgorod nchini Urusi kwa makini ingawa haikusiki kwa namna yoyote na tukio hilo. Podolyak amesema kwamba huenda makundi ya wapiganaji ya Urusi ndiyo yaliyohusika.