1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Urusi yadai kuvikamata vijiji viwili mashariki mwa Ukraine

21 Julai 2024

Urusi imesema kwamba vikosi vyake vimevikamata vijiji viwili vilivyo kwenye mstari wa mbele wa uwanja wa vita mashariki mwa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4iYYZ
Ukraine |
Gari la kijeshi limefichwa huku kukiwa na uharibifu huko, kijiji kilichokumbwa na mashambulizi makali:Picha: Narciso Contreras/Anadolu/picture alliance

Tangazo hilo limetolewa na wizara ya ulinzi ya Urusi kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Imevitaja vijiji hivyo kuwa ni Andriivka kilichopo katika mkoa wa Luhansk na Pishchane kwenye mkoa wa kaskazini mashariki wa Kharkiv.

Soma pia: Jeshi la Ukraine latofautiana kuhusu kukombolewa kwa Andriivka

Vijiji hivyo vinapakana kwa umbali wa kilometa 20 na vipo kwenye eneo la mstari wa mbele ambalo vikosi vya Urusi vimepata mafanikio makubwa na kusonga mbele katika siku za karibuni.

Hata hivyo sehemu ya maeneo ambayo Urusi imeyakamata ni yale yaliyotelekezwa na waakazi wake kutokana na mapigano yanayoendelea. Kijiji cha Andriivka kilikuwa na wakaazi wasiopindukia 20.

Moscow pia ilikuwa inakikodolea macho kijiji cha Pishchane kwa dhamira ya kufungua njia ya kuufikia mto Oskil.