SiasaUrusi
Urusi yachukua udhibiti wa vijiji viwili eneo la Kursk
11 Desemba 2024Matangazo
Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema vikosi vyake vimekomboa vijiji vya Darino na Plyokhovo katika operesheni zao.
Ukraine nayo imefahamisha kwamba imefanya mashambulizi kwenye maeneo ya mpakani na Urusi ya Rostock na Bryansk kwa makombora na droni Jumatano asubuhi, na kusababisha mripuko kwenye kituo kimoja cha mafuta na kusababisha uharibifu kwenye eneo hilo.
Kituo hicho kimeelezwa kwamba kilikuwa kinategemewa kwa shughuli za usafirishaji mafuta kwa wanajeshi wa Urusi.
Rais Volodymry Zelensky amesifia kipigo hicho dhidi ya Urusi akisema mashambulio hayo yatasaidia kuvifikisha mwisho vita vya Urusi.