Urusi yaapa kujibu vitisho kwenye mpaka wake wa Magharibi
9 Agosti 2023Matangazo
Waziri wa ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu amesema leo kwenye mkutano na maafisa wa kijeshi kwamba vitisho kwa usalama wa kijeshi wa Shirikisho la Urusi vimeongezeka katika maeneo ya kimkakati ya magharibi na kaskazini magharibi na kuongeza kuwa hatua hiyo inahitaji majibu yanayofaa.
Poland, mshirika mkubwa na jirani wa Ukraine imeimarisha usalama kwenye mipaka yake na Belarus baada ya Minsk kuwa makao mapya ya wapiganaji wa kundi la Wagner.
Katika hatua nyingine, Warsaw imetangaza itapeleka wanajeshi 2,000 zaidi kwenye mpaka wake wa mashariki kuungana na wanajeshi wengine 2,000 walioko kwenye eneo hilo.