Urusi, Ukraine zatupiana lawama kuanguka ndege ya wafungwa
25 Januari 2024Ijapokuwa wachunguzi wamedaiwa kupata visanduku vya kuhifadhi taarifa za safari siku moja baada ya kuanguka kwa ndege hiyo jana, kuna matumaini madogo ya kufahamu kilichosababisha tukio hilo huku kila upande ukitupiana lawama ijapokuwa hakuna aliyetoa ushahidi wa kuthibitisha hilo.
Ndege hiyo ilianguka katika eneo la Belgorod nchini Urusi na maafisa wakasema watu wote 74 waliokuwemo, ikiwa ni pamoja na wafungwa 65 wa kivita, waliuawa.
Soma zaidi: Ukraine yataka uchunguzi wa kimataifa katika ajali ya ndege ya Urusi
Urusi kupitia msemaji wa Ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov, inadai kuwa Kyiv iliidungua ndege hiyo na makombora mwili na kusema wafungwa hao wa kivita walikuwa njiani kwenda kubadilishwa na wa Urusi.
Ukraine ilijibu kwa kuituhumu Urusi kwa kusambaza propaganda.
Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine ametoa wito wa kufanywa uchunguzi wa kimataifa kuhusu tukio hilo