1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Urusi na Ukraine zahujumiana kwa droni na makombora

11 Agosti 2023

Miripuko kadhaa imesikika leo kwenye mji mkuu wa Ukraine, Kiev, baada ya maafisa kutangaza tahadhari ya mashambulizi ya anga nchini nzima.

https://p.dw.com/p/4V2VO
Uharibifu uliofanywa na kombora mjini Kyiv
Miji ya Ukraine imekuwa ikishuhudia mashambulizi ya kila wakati tangu Urusi ilipotuma vikosi vyake zaidi ya mwaka mmoja uliopitaPicha: Roman Petushkov/Xinhua/picture alliance

Maafisa wa Kiev wamesema kikosi cha anga kilikuwa kazini na kiliripoti kuwa Urusi imefanya mashambulizi ya makombora ya mwendo wa kasi kwenye mji wa Kiev.

Maafisa hao wamesema vipande vya kombora lililodunguliwa vimeanguka kwenye eneo la hospitali ya watoto, lakini hakuna majeruhi wala uharibifu.

Aidha, Urusi imesema imeiharibu ndege isiyo na rubani ya Ukraine katika viunga vya mji wa Moscow. Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema jaribio la Ukraine kufanya shambulizi la kigaidi limeshindikana.

Wakati huo huo, mji wa kihistoria wa Ujerumani wa Wurzburg, umetoa magari matatu ya kikosi cha zima moto kwa mji ndugu wa Lviv, baada ya kombora la Urusi kuushambulia mji huo mwezi Julai.